Rehema Juma Kishena (40) aliyekuwa anaomba msaada wa matibabu kutokana na uvimbe unaomsumbua kwa miaka 17 amefanikiwa kwenda hospitalini kwaajili ya matibabu, Akizungumza na mwandishi na Mwazilishi wa Vuka Initiative Bi. Vero Ignatus, dada wa Mgonjwa Aziza Bakari Muyai amesema tayari wamefika hospitali ya Muhimbili na wanatarajia majibu kutoka kwa madaktari watakao mhudumia mgojwa ili wafahamu hatua itakayofuata.