Mwanzilishi wa Mradi wa Vuka Initiative Bi Veronica Ignatus alisema kuwa “Vuka Initiative” ni mradi wenye kusudi la kupunguza changamoto za ukatili na unyanyasaji wa kijinsia katika jamii. Dira yake ni kuwa taasisi kimbilio kwa watu wote wenye changamoto za kimaisha.

Pia alisema kuwa Dhima yake ni kuifikia jamii na kutatua changamoto za ukaliti na unyanyasaji wa kijinsia ambapo Motto wao unaowaongoza ni “Vuka yako, Salama yako”

Bi Veronica alisema kuwa mradi huu unatarajia kuanza kufikia watoto na wanawake katika makundi ya wanawake yaani wafanyakazi wa sekta rasmi na zisizorasmi, mpango ni kuanzia na wilaya sita za mkoa wa Arusha.

Vuka Initiative umelenga kwa dhati kuisaidia serikali ya awamu ya tano ya Rais John Pombe Magufuli ya kuwaboreshea maisha na kuwawezesha wanawake na watoto.

Namna au mbinu ya kuifikia jamii itakuwa kwa kuandaa vipindi, warsha, semina, makongamano ya kuwafikia wanawake na Watoto.

Contact Info

HEAD OFFICE

Address: Makao Mapya Street, Arusha Tanzania.

Phone: +255 746 571 572

BRAND

Phone: +255 782 600 776

Newsletter

Subscribe to receive inspiration, ideas, and news in your inbox.

Address: Makao Mapya Street, Arusha , Tanzania.

© Vuka Initiative 2020. All Rights Reserved.