Katika kusheherekea sikukuu ya wanawake duniani 8/3 wazazi na walezi wametakiwa kujenga uhusiano wa karibu na Watoto wao na kutenga muda malezi na ufuatiliaji wa karibu mabadiliko ya tabia za watoto.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Bushbuck Safari Mustapha Panju alipokuwa akizindua mradi wa “Vuka Initiative” pamoja na uzinduzi wa kampeni ya  Mwogeshe Mwanao iliyofanyiaka katika Hoteli ya Corrido Spring mkoani Arusha.

Vuka Initiative itatumia kampeni ya “Mwogeshe Mwanao” kampeni hii inalenga kuwakumbusha wazazi na jamii kwa ujumla kuhusu jukumu la kuongeza ukaribu/mahusiano kwa watoto wao na kutenga muda wa malezi na ufuatiliaji wa karibu kwa Watoto wetu.

Vuka Initiative inatoa wito kwa jamii, vyombo vya habari na wadau mbalimbali kuunga mkono kwenye tukio na kuwa huru wakati wote kutoa ushauri, mapendekezo, maoni na michango ya hali na mali katika kuwezesha utekelezaji wa majukumu ya kuitumikia jamii na Taifa kwa ujumla.

Contact Info

HEAD OFFICE

Address: Makao Mapya Street, Arusha Tanzania.

Phone: +255 746 571 572

BRAND

Phone: +255 782 600 776

Newsletter

Subscribe to receive inspiration, ideas, and news in your inbox.

Address: Makao Mapya Street, Arusha , Tanzania.

© Vuka Initiative 2020. All Rights Reserved.