Kuhusu Vuka Initiative

Vuka Initiatives
Ni taasisi kimbilio kwa watu wenye changamoto za kimaisha. Tunajikita kuwafikia na kutatua changamoto ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia katika jamii.
Mwanzilishi wa Mradi wa Vuka Initiative Bi. Veronica Ignatus
alisema kuwa “Vuka Initiative” ni mradi wenye kusudi la kupunguza changamoto za ukatili na unyanyasaji wa kijinsia katika jamii , ambapo Motto wao unaowaongoza ni “Vuka yako, Salama yako” mradi huu unatarajia kuanza kufikia watoto na wanawake katika makundi ya wanawake yaani wafanyakazi wa sekta rasmi na zisizorasmi, mpango ni kuanzia na wilaya sita za mkoa wa Arusha.
Dhima Yetu
Kuifikia jamii na kutatua changamoto za ukaliti na unyanyasaji wa kijinsia.
Dira Yetu
Kuwa taasisi kimbilio kwa watu wote wenye changamoto za kimaisha.
Thamani Yetu
Tunajikita kuwafikia na kutatua changamoto za ukatili na unyanyasaji wa kijinsia katika jamii.
Tunalo Tumaini.